Part 2 baada ya msichana wa komba kupatikana: Fahamu yote kuhusu ukweli kuvuja kwa Picha zile.

SIKU chache zimekatika baada ya tukio la kusambaa mitandaoni kwa picha tata zenye pozi kati ya mheshimiwa Komba na mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Angel.


Angel Kissanga, mkazi wa Kinondoni jijini Dar anayedaiwa kupiga picha tata na mheshimiwa Komba.

Hatimaye mrembo huyo ameibuka na kuanika mambo mazito kama si makubwa, Risasi Mchanganyiko linakudadavulia.

Awali katika gazeti hili toleo la Jumamosi iliyopita ukurasa wa mbele kulikuwa na habari hiyo ikiwa na kichwa; KHAA! KOMBA! Katika habari hiyo picha zilizomuonesha mheshimiwa Komba akiwa na mrembo huyo zilipamba ukurasa huku mwenyewe (Komba) akidai ni picha za kutengeneza).

OFM YAINGIA MITAANI
Kwa vile Komba alikataa picha si zake huku baadhi ya vyombo vya dola kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) vikitangaza kuingia kazini kumtafuta sosi wa picha hizo, ilibidi timu makini ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kutoka Global Publishers iingie kazini kumsaka mrembo huyo kwa udi na uvumba.


Mheshimiwa Komba.

YATUMIA NUSU SIKU
OFM ambayo huwa haishindwi kitu, ilitumia nusu siku ya Ijumaa iliyopita na kufanikiwa kuinasa namba ya simu ya mkononi ya Angel pamoja na picha nyingine ikiwepo iliyotumika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Aidha, ilibainika kwamba, mrembo huyo anaitwa Angel Kissanga, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, bila ajizi Paparazi wetu alimwendea hewani Angel na kumuuliza kama ana habari zozote kumhusu yeye.
Angel: “Habari kama zipi? Mimi sina habari zozote.”

Paparazi: “Hujaona kwenye mitandao ya kijamaii wameweka picha zako ukiwa katika mapozi tata na mheshimiwa Komba?”
Angel: “Ngoja kwanza, nitakupigia.”

MUDA UNAKWENDA, ANGEL ARUDIWA
Baada ya kuona muda unakatika bila mrembo huyo kupiga simu kama alivyokuwa ameahidi, paparazi wetu alimrudia hewani ambapo safari hii simu yake ilipokelewa na mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni dada wa Angel.




Angel Kissanga katika pozi na mheshimiwa.

“Mimi si Angel, ni dada yake. Angel amepandwa na presha baada ya wewe kumwambia kuna picha zake na mheshimiwa Komba kwenye mitandao.
“Unajua ngoja nikuambie ukweli. Mdogo wangu ameshtuka sana, hivi hapa tupo Hospitali ya Micco Sinza, amelazwa.”

PAPARAZI ATIA TIMU HOSPITALINI
Kusikia hivyo, paparazi wetu alifunga safari hadi kwenye hospitali hiyo ambapo kweli mrembo huyo alikuwa amelazwa kwa matatizo ya presha ya kupanda.

Mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mama mdogo wa Angel alimjia juu paparazi wetu akidai yeye ndiyo chanzo cha mwanaye huyo kupandwa na presha ghafla, akamtimua asimuone mgonjwa.

MAZUNGUMZO YA BAADAYE
Siku iliyofuata, paparazi alibahatika kuzungumza na Angel ambaye aliweka wazi mambo yake kuhusu picha hizo kama ifuatavyo:

“Mimi nataka kusema kwamba picha nimeziona, nazifahamu kweli ni mimi.”
Paparazi: “Ni kweli ulipigwa ukiwa na mheshimiwa Komba?”
Angel: “We jua tu kwamba picha nazijua. Zilipigwa na simu ya LG.”
Paparazi: “Alipiga nani?”

Angel: “Nimesema nazifahamu.”
Paparazi: “Hiyo simu ni ya nani?”
Angel: “We wa nini?”





Angel Kissanga.

Paparazi: “Okey, mheshimiwa Komba unamfahamu?”
Angel: “Namfahamu ndiyo.”
Paparazi: “Ni nani wako?”

Angel: “Nimekwambia namfahamu.”
Paparazi: “Sasa mbona mheshimiwa Komba anasema picha zimetengenezwa?”
Angel: “Mimi sijui sasa.”

ANGEL ATAKIWA KUTIA TIMU GLOBAL
Baada ya mazungumzo hayo, paparazi alimtaka msichana huyo kufika kwenye ofisi za magazeti ya Global ambapo alikubali.

Hata hivyo, baadaye alisema amebatilisha baada ya baba yake kuingilia kati sakata la picha hizo akidai yeye ndiye atakuwa msemaji mkuu.
Habari za chini kwa chini zilidai kwamba, kusita kuweka miguu kwa Angel kwenye ofisi za Global kulitokana na zuio la mheshimiwa mmoja ambaye alimchimba mkwara kwamba asitoe ushirikiano wowote na vyombo vya habari.

MASWALI MUHIMU
Maneno ya Angel na mheshimiwa Komba yanapingana. Mmoja anasema picha zilitengenezwa, mwingine anazitambua na zilipigwa kwa simu ya LG, nani mkweli?

ANATAJWA PAULINA
Mbali na kupishana kwa maneno ya wawili hao, mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Paulina anatajwa kuwa nyuma ya sakata hilo.

Mwanamke huyo anadaiwa wakati fulani kuingia kwenye mzozo na Angel na akaja kudai ameipata simu yenye picha za mrembo huyo na mheshimiwa bila kujulikana alikoipata. Je, aliipata kwa Angel au mheshimiwa Komba?

Ni mzozo gani aliokumbana nao Angel kwa Paulina? Unaweza kuwa wa wivu wa mapenzi? Na kama ni wivu wa mapenzi walikuwa wanamgombea nani?


UTATA KUHUSU KOMBA
Katika mahojiano na Risasi, Komba alipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, Alhamisi mchana wa saa 7 baada ya kutoka bungeni, kabla ya kuelezwa sababu za kupigiwa simu, alijibu anajua alichopigiwa simu. Alijuaje?

Aidha, Komba alisema anazijua zile picha lakini yule msichana hamtambui.
Komba alisema anazo picha nyingine akiwa kwenye pozi la kawaida bila yule msichana, alipotakiwa kuzituma kwa mwandishi ili ajiridhishe, alikataa!

Achana na maneno ya kwenye mitandao ya kijamii, Komba alipohojiwa na kituo kimoja cha redio, Ijumaa asubuhi, akasema anajua zile picha zimetengenezwa na wabaya wake, lakini akasema anamwachia Mungu. Kwa nini amwachie Mungu jambo zito kama hilo?

MAGAZETI YA GLOBAL
OFM ni kitengo rasmi, makini kilicho ndani ya Global. Hakijawahi kushindwa. Kimefichua uovu mwingi sana unaofanyika kwenye jamii. Kwa hili la Komba na Angel, ni dogo sana. Tunaahidi kuendelea kufuatilia na tutaanika ukweli halisi wa kila kinachoendelea.

Magazeti pendwa ya Global ni Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi na Risasi. Hakikisha hukosi nakala yako. Tutakuwa wa kwanza kukuhabarisha ukweli halisi pengine kabla hata ya vyombo vya dola venye kila aina ya vifaa.





  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Huyu ndio mshindi kwenye shindano la wenye hipsi kubwa.



Ijeoma Nnaj ndio msichana aliyebahatika kulitwaa taji hilo la msichna mwenye mahips na matako makubwa na kubahatika kuzawadia gari jipya.



Hawa ndio washiriki wote wakiwa katika picha ya pamoja.



Mmoja wa mshiriki akiwa mbele ya majaji.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Part 2:Fahamu kilichojili nyuma ya panzia juu ya kifo cha nyoka mkubwa Arusha.

Jamani mungu atupe imani katika hii dunia jamni baba huyo mnaemuona hapo kafanya ushirikina ili apate mali na awetajiri sana hapa duniani bila ya kufikiria km kesho kwa mungu atajibu nini akamchukua mtoto wake alie mzaa na kumgeuza nyoka na kumfungia ndani kwa muda wa miaka kadhaaa nasiku ya jana m.mungu akataka kudhalillisha kwa shirki anayofanya,huwa wakienda kusafisha na kumuekea chakula nyoka huyo anafungua dirisha ili hewa iingie na sasa akawa amesahau kufunga dirisha,ndio chanzo cha yule nyoka akatoka nje na majirani wakaanza kupiga kelele bila kujua kinachoendelea.
 Hatimae wanaume wakajitokeza na kumuuwa na baada ya muda mfupi watu wa pale nyumbani kwake wakampigia cm kuwa kunanyoka mkubwa ametoka chumba kile unacho sema asiingie mtu na majirani wamemuuwa palepale yule bwana aliacha shughuli alizokuwa akifanya na kuja katika sehemu ya tukio na kuwakuta watu wamekusanyika na hapo tayari walisha muuwa nyoka huyo jamaaa akionyesha anauchungu na kuanza kusema kwa hisia kali mm sasa ntakuwa maskini,na ni nani aliewaambie mumuuwe nyoka huyu hali ya kuwa hiii ni dawa ya mali yangu na huyu ni mtoto wangu mimi nimembadilisha awe hivi jamani,bila kujali ni mbele za watu na anachozungumza ni nini subhana llwah hapo ndipo watu wakaijua siri ya baba huyo na nn kilikuwa kinaendelea.
Hiki ndio hasa kilichotokea Arusha.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Msichana atembea uchi sinza.

  
 
Akizua timbwili kwa wananchi waliokuwa eneo hilo.
TIMBWILI! Mrembo wa haja ambaye jina halikupatikana mara moja, amenaswa akiwa matiti ‘nido’ nje baada ya kulewa tilalila mchana kweupe na kulizwa mkoba wake kisha kuzua varangati ‘hevi’.

Mrembo akidhibitiwa baada ya kuzua timbwili.Varangati hilo lililonaswa na kachero wetu aliyekuwa kwenye ‘patroo’ ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM), lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza- Afrika Sana jijini Dar.

Katika sinema hiyo ya bure, mrembo huyo alishuhudiwa akipigana na kila mtu aliyekutana naye mbele yake huku akivua nguo kuashiria kuwa ‘pombe si chai’.
 
..Akitulizwa na wananchi. Kuna wakati mwanadada huyo alikatiza barabarani bila kujali magari na nusura agongwe jambo lililosababisha mtafaruku wa foleni huku mwenyewe akidondoka kama ‘embe dodo’ lililoiva.


...Akionyesha kutokubaliana nao na kuzidi kukinukisha.Baada ya timbwili hilo kuchukua takriban dakika 35, ilibidi wasamaria wema kuingilia kati na kumshika huku akiwapiga baada ya kuona huenda angeumizwa.


...Akiwa chini nido nje.Baadaye watu hao walifanikiwa kumtoa eneo la barabara huku wakimsitiri kwa kupandisha nguo kufunika nido kisha kumpeleka pembeni na kumtuliza.
“Kweli pombe siyo chai. Yaani msichana mzuri lakini ona alivyojidhalilisha,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.
  ...Akiondoka huku nido zake zikiwa wazi.Paparazi wetu alitaka kujua kulikoni kuwa katika hali hiyo ambapo mrembo huyo alijibu kwa kifupi kuwa kuna mtu alimuibia mkoba wake hivyo akawa hana namna nyingine zaidi ya kufanya fujo kutokana na hasira.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Baada ya kubadili dini:Royal Prince wa Kuwaita Abdulah ahofiwa kuuangusha ufalme wa kiislam arabuni Moto wawaka.



Katika faili la sauti iliyotolewa na Mkristo satellite TV channel, Peince Abdullah al-Sabah alitangaza imani yake katika Yesu Kristo.
Waislamu kushambuliwa kwake kusema "yeye si mwanachama wa familia ya kifalme"

Kulingana na taarifa, Kuwaiti Royal Prince mekuwa mfuasi wa Yesu Kristo. Katika faili la sauti posted na jina lake, yeye unathibitisha kwamba kama yeye ata  uawa kwa sababu ya rekodi alioifanya ambayo yenye mazungumzo juu ya kuokolewa kwake, ana imani kuwa atakutana Yesu Kristo uso kwa uso.

 Habari kunatokana na Mashariki ya Kati ambayo hali ya kuwa al-Haqiqa - Christian satellite TV channel ya Kiarabu inayoambukiza mipango ya dini ya kikristo - matangazo faili la sauti kuhusishwa na mkuu Kuwaiti, kutambuliwa kama Abdullah al-Sabah. al-Sabahs ni familia ya kifalme ya Kuwait, nchi tajiri kwa mafuta. jina Abdullah (mtumishi wa Mungu) mara kwa mara inaonekana katika Emir familia ya mti.
Katika Sanjari wake redio, Abdullah alisema:

"Awali ya yote, mimi kikamilifu kukubaliana na usambazaji wa hii faili la sauti na Mimi sasa natangaza kwamba kama wao kuniua kwa sababu ya hiyo, basi mimi itaonekana kabla ya Yesu Kristo na kuwa pamoja naye kwa milele yote ".

 Katika taarifa hiyo, mkuu inaonyesha ufahamu wake juu ya hatima ya katika duka kwa shahidi wa imani, kwa mujibu wa mafundisho ya Kikristo. televisheni alisema kuwa Abdullah ni mwanachama wa familia ya kifalme, na kwamba yeye hivi karibuni tumekataa imani yake katika Uislamu na kuwa Mkristo, bila kufafanua ambayo hasa tawi la Ukristo alikuwa kuchaguliwa. Baada ya kusema jina lake kamili, mkuu alisema:
"mimi kukubali chochote kufanya kwangu, kwa sababu ukweli katika Biblia ameniongoa kwenye njia ya haki."
Prince Abdullah Al Sabah ndie anaye fuata katika ufalme wa Kuwait. Kuwait kwa mara ya kwanza inaweza ikapata Mfalme ambaye ni Mkristo, jambo ambalo litatikisa falme na nchi nyingi za kiarabu!

Katika faili la sauti, Abdullah amezungumzia  juu ya makundi ya Kiislamu kuwa ni yanayoshindaa uchaguzi katika Misri na anatangaza hivi: "jumuia za Kiislamu siku zote inatakaa kushambulia katika sehemu mbalimbali za dunia lakini Mungu ana tulindwa dunia na bado anailinda. Hii ni kwa nini sisi hivi karibuni kuonekana kutoelewana kuonekana kati ya vikundi vya Kiislamu ambao sasa kupambana na kila mmoja. Wao ni kuhusu kugawanya zaidi katika makundi tofauti. "

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Mwenyekiti wa Baraza la maimamu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris auawa kwa risasi.


Mwenyekiti wa baraza la maimam na muhubiri maarufu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa.

Sheikh Mohammed Idris ameuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumbani kwake eneo la Likon baada ya kuvamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha, wakati akitoka nyumbani kuelekea msikitini.

Taarifa kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa Sheikh Mohammed Idris alikuwa akipata vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa kundi la vijana wa kiisilamu wanaodai mabadiliko, na amewahi kutoa taarifa za vitisho hivyo na kusema kuwa anahofia maisha yake.

Decemba mwaka jana Sheikh Idris na mpinzani wake Mohamed Khalifa walinusurika kifo baada ya msikiti wao kuvamiwa na vijana zaidi ya 100, ambao walitawanywa na polisi.

Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya kumbukumbu ya Pandya, mjini Mombasa

Pamekuwa na matukio ya mara kwa mara ya mauaji ya viongozi maarufu wa dini katika mazingira ya kutatanisha.


  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Walioitwa katikas usaili serikalini kuanzia june 14 hadi 21 mwaka huu.



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/G/25 07 Juni, 2014

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango, Geological Survey of Tanzania (GST) na Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs), anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanywa kabla ya usaili kuanza.
2. Usaili wa ana kwa ana utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Wafike na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Wafike na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8. Kila msailiwa azingatie muda, tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
12. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama ilivyooneshwa kwenye tangazo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS