Dida wa Times Fm:Mume wangu alitumia mkanda wa suruali kuniadhibu.


Hizi ni picha zikionyesha majeraha aliyopata mtangazaji wa kituo cha Times FM,Khadija Shaibu maarufu kama Dida baada ya kupata kipigo kikale kutoka kwa mume wake Edzen Jumanne.




Mtangazaji huyo alipata kipigo kikali toka kwa mume wake baada ya kuibuka mzozo mkubwa unaodaiwa kuwa chanzo chake ni wivu tu aliokuwa nao mume wake.

Dida alifunguka kwa kusema majeraha hayo yanatokana ni kipigo kikali cha mume wake ambae alitumia mkanda wake wa suruali kotolea kipigo hicho.Aidha taarifa za awali toka kwa watu wake wa karibu aka wapambe zinasema kuwa ndoa ya wapendanao hao iko matatani tokea kuibuke sakata ilo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Uharifu utaisha: Silaha aina ya AK 47 zaingia Tanzania.







Silaha za kivita zikiwamo za AK 47, SMG na nyingine zimekuwa zikiingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya, imeelezwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amesema silaha hizo zimekuwa zikiingia nchini kinyemela kupitia vichochoro ambavyo ni vigumu kuvidhibiti kutokana na mazingira yake.

Ndugu yangu mwandishi suala la hapa mpakani lina changamoto zake… kuhusu silaha kuingia Tanzania kutoka Kenya hilo lipo si kwamba zinangia kwetu la hasha nyingine zinatoka Tanzania kwenda Kenya.

“Tatizo lililopo ni kwamba koo zote zilizopo Mkoa wa Mara zipo Kenya, sasa ni vigumu kumjua huyu ni rai wetu au siyo. Jambo jingine linalosababisha ugumu katika kudhibiti hali hii ni ushirikiano uliopo kati ya raia wa Kenya na Tanzania.

“…yaani huwezi kuwatambua kama ni lugha zote wanazijua, lakini kwa upande wetu wa polisi tumekuwa tukifanya operesheni kila mara na kwa mwezi tunaweza kukamata bunduki mbili hadi nne.

“Changamoto kwetu polisi ni kunyimwa taarifa kutoka kwa wananchi, koo za huku Tarime zina hali ile ya ujasiri na usiri mkubwa. Tunachowaomba wananchi watoe taarifa kwetu kwa sababu silaha hizo ni hatari kwa usalama wao na mali zao,”alisema.

Kamugisaha alisema polisi wanaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi vya Kenya katika kudhibiti vitendo vya uhalifu mpakani ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wanaobahatika kukamatwa.Ametoa kauli hiyo baada ya kuwapo malalamiko ya wananchi juu ya silaha nzito kuingiza nchini kupitia mpakani mwa Tanznaia na Kenya jambo ambalo linawapa wasiwasi ya usalama wao.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS