Dida wa Times Fm:Mume wangu alitumia mkanda wa suruali kuniadhibu.


Hizi ni picha zikionyesha majeraha aliyopata mtangazaji wa kituo cha Times FM,Khadija Shaibu maarufu kama Dida baada ya kupata kipigo kikale kutoka kwa mume wake Edzen Jumanne.




Mtangazaji huyo alipata kipigo kikali toka kwa mume wake baada ya kuibuka mzozo mkubwa unaodaiwa kuwa chanzo chake ni wivu tu aliokuwa nao mume wake.

Dida alifunguka kwa kusema majeraha hayo yanatokana ni kipigo kikali cha mume wake ambae alitumia mkanda wake wa suruali kotolea kipigo hicho.Aidha taarifa za awali toka kwa watu wake wa karibu aka wapambe zinasema kuwa ndoa ya wapendanao hao iko matatani tokea kuibuke sakata ilo.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Uharifu utaisha: Silaha aina ya AK 47 zaingia Tanzania.







Silaha za kivita zikiwamo za AK 47, SMG na nyingine zimekuwa zikiingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya, imeelezwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amesema silaha hizo zimekuwa zikiingia nchini kinyemela kupitia vichochoro ambavyo ni vigumu kuvidhibiti kutokana na mazingira yake.

Ndugu yangu mwandishi suala la hapa mpakani lina changamoto zake… kuhusu silaha kuingia Tanzania kutoka Kenya hilo lipo si kwamba zinangia kwetu la hasha nyingine zinatoka Tanzania kwenda Kenya.

“Tatizo lililopo ni kwamba koo zote zilizopo Mkoa wa Mara zipo Kenya, sasa ni vigumu kumjua huyu ni rai wetu au siyo. Jambo jingine linalosababisha ugumu katika kudhibiti hali hii ni ushirikiano uliopo kati ya raia wa Kenya na Tanzania.

“…yaani huwezi kuwatambua kama ni lugha zote wanazijua, lakini kwa upande wetu wa polisi tumekuwa tukifanya operesheni kila mara na kwa mwezi tunaweza kukamata bunduki mbili hadi nne.

“Changamoto kwetu polisi ni kunyimwa taarifa kutoka kwa wananchi, koo za huku Tarime zina hali ile ya ujasiri na usiri mkubwa. Tunachowaomba wananchi watoe taarifa kwetu kwa sababu silaha hizo ni hatari kwa usalama wao na mali zao,”alisema.

Kamugisaha alisema polisi wanaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi vya Kenya katika kudhibiti vitendo vya uhalifu mpakani ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wanaobahatika kukamatwa.Ametoa kauli hiyo baada ya kuwapo malalamiko ya wananchi juu ya silaha nzito kuingiza nchini kupitia mpakani mwa Tanznaia na Kenya jambo ambalo linawapa wasiwasi ya usalama wao.

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Unaikumbuka hii:Mwanamuziki maarufu aumbuka stajini baada ya gauni kuegea.


Hizi ndio picha za tukio zima lilivyokuwa likiendelea.






  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Sister wa kanisa auwawa katika sambulio la majambazi Ubungo.




SISTA wa Parokia ya Makoka iliyopo Kibangu, Dar ameuawa na majambazi yaliyokuwa kwenye bodoboda wakati akiingia kwenye gari akitokea dukani eneo la River Side, Ubungo jijini Dar es Salaam hivi punde. Kabla ya kuuawa sista huyo, dereva wake alipigwa risasi mkononi na majambazi hayo.





Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi.


Kidole cha dereva kilichokatwa kwa risasi.


Ganda la risasi likiwa eneo hilo la tukio.


...Dereva akiwasiliana na jamaa zake baada ya kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.


Wananchi wakiwa eneo la tukio.




SOURCE: GPL





  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

beib wa word cup hoi.






World cup hii
Demu; Baby kwanini hawa blue(Bosnia) wamefunga 2 na hawa akina Messi(Argentina) wamefunga 1 lkn inaonyesha akina Messi wameshinda mechi?
Jamaa; hawa blue goli 1 wamejifunga
Demu; kwahiyo lzm wafunge goli la huku?
Jamaa; ndiyo
Demu; sasa mbona Messi nae kafunga goli la huku?
Jamaa; halftime huwa wanabadilishana magoli
Demu; aanhaaa kumbe!!!
Demu; halaf baby si ulinambia uwanjani wachezaj mwisho 11?. sasa mbona yule kavaa no 15?
Jamaa; jezi unavaa no yoyote
Demu; sasa baby km golikipa anaruhusiwa kushika mpira na mkono kwanini asikimbie nao mpk mbele kisha akampa Messi akafunga lkn mpk apige huku huku?
Jamaa; mpenzi hebu tulale mpira umeshaisha kesho kazini

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

Mkoani Mtwara:Watoto wachezea bomu .



Jambo lisilo kuwa akawaida katika kata ya Mawala mkoani Mtwara Vijijini watoto walikutwa na msamalia mwema wakichezea bomu la 60mm walilolokota pembezoni na kichaka.



Baada ya msamalia huyo kuona ni kitu chenye umbo linalifanana na bomu aliamua kutoa taarifa polisi kabla ya wanajeshi kuja kulichukua kwa usalama zaidi.



  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS

EMMANUEL MBASHA AACHIWA KWA DHAMANA!






Muimbaji wa dini, Emmanuel Mbasha (ambaye ni mme wa Flora Mbasha) anayekabiliwa kwa kesi ya ubakaji, ameachiwa kwa dhamana na kesi itatajwa tena julai 17.
Emmanuel Mbasha amefikishwa leo mahakama ya Ilala na kupatiwa dhamana hiyo baada ya kutimiza masharti yaliyohitajika.

Bwana Emmanuel Mbasha alifikishwa mahakamani hapo kwa shitaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 anayedaiwa kuwa shemeji yake

  • Digg
  • Del.icio.us
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • RSS